• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 19 wauawa katika milipuko iliyotokea kwenye tamasha la muziki Manchester

    (GMT+08:00) 2017-05-23 09:19:30

    Polisi nchini Uingereza wamethibitisha kuwa milipuko miwili iliyotokea jana usiku kwenye tamasha la muziki mjini Manchester, imesababisha vifo vya watu 19 na wengine 50 kujeruhiwa.

    Taarifa iliyotolewa na polisi wa Manchester inasema wanachukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi, hadi taarifa zitakapothibitisha vinginevyo.

    Habari zinasema polisi waliitwa katika eneo hilo saa nne na dakika 35 usiku, baada ya taarifa kuhusu milipuko kwenye eneo hilo wakati tamasha linaendelea. Ukumbi wa Manchester Arena una uwezo wa kupokea watu elfu 21, na wakati wa milipuko ukumbi huo ulikiwa umejaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako