• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yawarudisha wakimbizi wa Somalia 64,761 kutoka Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-23 09:28:28

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNCHR limesema wakimbizi 64, 761 wa Somalia wamerudishwa nchini kwao tangu kazi ya kurudisha wakimbizi wanaotaka kurudi kwa hiari ianze mwaka 2014.

    UNHCR imesema kwenye taarifa inayotolewa kila baada ya wiki kuwa kati wakimbizi hao, wakimbizi 63,535 walirudishwa kutoka kambi ya Dadaab.

    Wakimbizi zaidi ya 1,400 walisaidiwa kurudi kwa ndege kutoka Dadaab, na wengine zaidi ya elfu 24 wamerudi wenyewe kwa mwaka huu. Wengi wa wakimbizi wametajwa kurudi katika miji ya Kismayu, Mogadishu na Baidoa.

    Hata hivyo idadi ya wasomali wanaorudi nyumbani kwa hiari imepungua. Sababu zilizofanya idadi hiyo ipungue zimetajwa kuwa ni ukame unaoendelea, mlipuko wa kipindupindu na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako