• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan, UN na AU zaidhinisha kuondolewa kwa kikosi cha UNAMID huko Darfur

    (GMT+08:00) 2017-05-23 09:32:41

    Kamati ya pande tatu kati ya serikali ya Sudan, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika imeidhinisha mpango wa pamoja unaotaka kuondolewa taratibu kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika cha kulinda amani huko Darfur UNAMID kwenye maeneo mengi ya Darfur.

    Kamati hiyo iliyoundwa mwezi Februari 2015, ilikutana jana huko Khartoum na kuangalia tena hali ya Darfur, ikilenga mkakati wa kuondolewa kikosi hicho katika eneo hilo na hatimaye kusaini makubaliano ya pamoja. Makubaliano hayo pia yanasisitiza kuboreshwa kikamilifu kwa usalama na hali ya kibinadamu katika majimbo yote ya Darfur.

    Tume ya UNAMID ina watumishi zaidi ya elfu 20, na inatajwa kuwa ni ya pili kwa ukubwa baada ya tume ya Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako