• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yafanya mazungumzo ya kitaifa

    (GMT+08:00) 2017-05-23 09:44:49

    Sudan Kusini ilifanya mazungumzo ya kitaifa jana huko Juba, ambapo rais Salva Kiir alitangaza kuwa serikali itasimamisha vita kwa upande mmoja.

    Akihutubia kwenye ufunguzi wa mazungumzo hayo, rais Kiir Amesema kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa kuna maana muhimu kwa ujenzi na utulivu wa Sudan Kusini, kutaweka jukwaa la kuondoa tofauti na kuhimiza maafikiano kati ya pande zinazopambana nchini Sudan Kusini, na pia kutasaidia kutatua masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yanayoikabili Sudan Kusini.

    Rais Kiir amesema lengo la kutangaza kusimiamisha vita ni kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mazungumzo ya kitaifa, na kutoa usalama kwa watoa misaada ya binadamu ya kimataifa. Amesema jeshi la ukombozi la umma la Sudan limeanza kutekeleza uamuzi wa kusimamisha vita tarehe 22, lakini litaendelea kuwa na haki ya kujilinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako