• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 70 wa afya duniani wafunguliwa Geneva

    (GMT+08:00) 2017-05-23 09:49:58

    Mkutano wa awamu ya 70 wa afya duniani ulifunguliwa jana asubuhi kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva. Kwenye mkutano huo wa siku kumi wawakilishi wa nchi 194 wanachama wa Shirika la afya duniani WHO watajadili masuala ya msingi ya afya, na kuchagua mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo.

    Katika ufunguzi wa mkutano huo, mjumbe wa Uswisi ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Bw. Alain Berset alimshukuru mkurugenzi mkuu wa WHO Dk. Margaret Chan, kwa juhudi na mchango wake katika kutokomeza ugonjwa wa Polio na kuliongoza shirika hilo kukabiliana na matukio zaidi 600 ya dharura ya kiafya kila mwaka..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako