• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa ripoti kuhusu shughuli za China katika Antaktika

    (GMT+08:00) 2017-05-23 10:03:02

    Idara ya bahari ya China imetoa ripoti kuhusu shughuli za China katika bara la Antaktika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya China kutoa ripoti rasmi kuhusu maendeleo ya shughuli za China katika eneo la Antaktika.

    Ripoti inasema, China imejenga kwa hatua ya kwanza mtandao wa kupima na kusimamia eneo la Antaktika na jukwaa la kutoa huduma kwa ajili ya uchunguzi katika sehemu hiyo linalohusisha meli ya uchunguzi "Chinare" na vituo vinne vya uchunguzi. Vilevile, kiwango cha uchunguzi wa kisayansi wa China kuhusu bara la Antaktiki kimeendelea kuinuka.

    Ripoti pia inasema Katika muda wa zaidi ya miaka 30 tangu kikosi cha kwanza cha uchunguzi wa Antaktika cha China kilipotumwa mwaka 1984, shughuli za utafiti za China katika eneo hilo zimepata mafanikio makubwa. Katika siku za baadaye, China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, katika kusukuma mbele ujenzi wa utaratibu wa kimataifa kwenye bara la Antaktika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako