• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump asema Iran inatakiwa kuishukuru Marekani kwa manufaa inayopata kutokana na makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2017-05-23 10:11:07

    Rais Donald Trump wa Marekani ameshambulia makubaliano ya kinyuklia na Iran, huku akiwaambia wanahabari nchini Israel kuwa Iran inatakiwa kuishukuru Marekani kwa manufaa iliyoyapata kutokana na makubaliano hayo.

    Rais Trump amesema Marekani imewapa mali na ustawi na uwezo wa kuendelea na ugaidi, lakini amesisitiza kuwa kamwe Iran haitafanikiwa kutengeneza silaha za nyuklia.

    Habari zinasema, rais Hassan Rouhani wa Iran ameitaka Marekani ifikirie upya sera ya kiadui dhidi ya Iran. Amesema, sera hiyo siku zote inashindwa, ikiwemo kuiwekea Iran shinikizo na vikwazo, huku akisisitiza kuwa licha ya mipango ya kunufaishana, Marekani haina chaguo lingine katika uhusiano kati yake na Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako