• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 10 wauawa katika shambulizi lililofanywa na kundi la Taliban katika kambi ya jeshi kusini mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-05-23 16:36:31

    Askari 10 wa Afghanistan wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa kundi la Taliban kwenye kambi ya jeshi iliyoko Kandahar, kusini mwa Afghanistan, usiku wa kuamkia leo.

    Hata hivyo wapiganaji hao walishindwa kuingia ndani ya kambi baada ya vikosi vya ziada kufika eneo la tukio mara baada ya mapambano kuanza, ambapo wapiganaji kadhaa wa kundi la Taliban waliuawa na wengine kujeruhiwa.

    Kundi la Taliban limekuwa likifanya mashambulizi mfululizo tangu mwezi uliopita wakati wapiganaji wa kundi hilo walipozidisha mashambulizi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako