• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Cote'd Ivorie akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2017-05-23 16:47:25

    Rais Alassane Ouattara wa Cote'd Ivorie amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi katika ikulu ya nchi hiyo mjini Abidjan.

    Katika mazungumzo yao, Rais Ouattara amesema, ushirikiano wa sekta mbalimbali kati ya China na Cote'd Ivorie unaendelea kuimarishwa, na urafiki kati ya nchi hizo ni mfano wa kuigwa kati ya China na nchi za Afrika. Amesema Cote'd Ivorie inajionea fahari kuwa na mwenzi wa kutegemeka kama China.

    Kwa upande wake, Bw. Wang amesema, ushirikiano kati ya pande hizo mbili unaendelea vizuri, na China imekuwa nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini Cote'd Ivorie na pia imechukua nafasi ya tatu katika biashara. Amesema China inapenda kusaidia Cote'd Ivorie kuharakisha mchakato wa mageuzi ya kiviwanda na kulinda haki na maslahi halali ya nchi za Afrika na nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako