Kampuni mpya ya sukari ya Kwale imegeuka kuwa mojawapo ya kampuni kubwa zaidi za sukari hapa nchini Kenya kutokana na matumizi teknolojia ya kisasa.
Kampuni hiyo Inaweza kusaga tani elf-3 za miwa kila siku.
Kampuni hiyo iliyojengwa katika ardhi ya hekta-5,500 katika kaunti ya Kwale inategemea zaidi kilimo cha unyunyiziaji maji kwenye upanzi wa miwa.
Kampuni ya sukari ya Kwale imekuwa ikivuna tani-60 za miwa inayotegemea maji ya mvua na tani-140 za miwa inayokuzwa kwa njia ya unyunyiziaji maji. Meneja wa shughuli kwenye kampuni hiyo, Ravi Chandra amesema kampuni hiyo imekuwa ikiuza sukari iliyopakiwa kwenye mifuko ya kilo-50 na sasa itauza sukari katika pakiti za kilo moja, kilo mbili na hata gramu mia tano na mia mbili hamsini kabla ya mwisho wa mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |