• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Museveni aongeza mda wa usajili wa kadi za simu za rununu

    (GMT+08:00) 2017-05-23 18:55:46

    Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ameongeza mda wa makataa wa kusajili laini za simu za mkononi.

    Museveni ameafikia uamuzi huo baada ya mazungumzo na bunge na kamati ya mawasiliano nchini humo.

    Museveni amesema kwamba wateja wote wa simu za mkononi watatakiwa kuendelea na usajili wa simu hizo kabla tarehe 30 Agosti mwaka 2017.

    Waziri wa mawasiliano Frank Tumbwebaze amewaonya wateja ambao watakosa kusajili laini zao kuchukuliwa hatua za kisheria.

    Amri hii imefikishwa katika kampuni zote za huduma za mawasiliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako