• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo mpya wa ushuru wapongezwa

    (GMT+08:00) 2017-05-23 18:55:46

    Halmashauri ya ushuru ya Rwanda imepongeza mpango mpya wa wahudumu wa uchumi wa ukusanyaji ushuru katika maeneo ya mipaka.

    Rosine Uwamariya meneja wa oparesheni wa halmashauri hiyo amesema mfumo huo utachangia uwazi wa biashara.

    Aidha biashara katika sehemu za mipaka itarahisishwa kufuatia utaratibu wa kasi wa ulipaji ushuru.

    Jumuiya ya kanda ya Afrika Mashariki imeidhinisha utekelezaji wa sheria mpya ya ushuru wa kikanda itakayohamasisha uwiano kibiashara.

    Wamiliki wa kampuni za uagizaji na uingizaji wa bidhaa kutoka Rwanda hadi nchi za nje watafaidika na mpango huu wanaodai utainua mapato na kupunguza rushwa za uchukuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako