• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sportpesa yaendelea kudhamini vilabu vya soka Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-05-24 09:27:12

    Kampuni ya SportPesa jana imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Singida United kwa dau la Sh. Milioni 250.

    Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema kwamba wameingia mkataba na timu hiyo kwa sababu imeonyesha nia ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

    Tarimba amesema kwamba mkataba huo una kipengele cha kuongezwa iwapo Singida United itafanikiwa kubaki Ligi Kuu baada ya msimu ujao.

    Kwa upande wake, kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba udhamini huo ni chachuya timu kufanya vizuri msimu ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako