• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Laurent Koscielny kuikosa fainali ya kombe la FA

    (GMT+08:00) 2017-05-24 09:29:41

    Laurent Koscielny ataikosa mechi ya fainali ya FA CUP ya Timu yake Arsenal ambao watacheza na mabingwa wa England Chelsea Jumamosi hii uwanjani Wembley Jijini London.

    jana, Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwa Rufaa ya Arsenal ya kupinga kufungiwa Mechi 3 kwa Beki wao huyo imetupwa. Koscielny alitolewa nje kwa kadi nyekundu Jumapili iliyopita uwanjani Emirates baada kumchezea rafu mbaya Enner Valencia wakati wa mechi yao ya mwisho ya msimu wa EPL, walipoitwanga Everton 3-1.

    Sasa Koscielny atatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 3 na inaanza mara moja na mechi ya kwanza kuikosa ni hiyo fainali ya kombe la FA.

    Mechi nyingine ambazo Koscielny atazikosa ni zile mbili za kwanza za Arsenal za msimu mpya wa ligi ya Uingereza 2017/18 ambazo zitaanza Agosti 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako