• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Brussels waimarisha usalama kabla ya ziara ya rais wa Marekani na mkutano wa kilele wa NATO

    (GMT+08:00) 2017-05-24 10:11:08

    Meya wa mji wa Brussels Bw. Yvan Mayeur amesema, mji huo utakuwa katika kiwango cha juu zaidi cha usalama kutokana na ziara ya rais Donald Trump wa Marekani nchini Ubelgiji na mkutano wa kilele wa Jumuiya ya NATO.

    Bw. Mayeur amesema, kabla ya mkutano wa NATO, hatua za ngazi za juu za usalama zimechukuliwa mjini humo, na polisi zaidi ya elfu 4 watafanya doria kote mjini.

    Habari zinasema rais Donald Trump wa Marekani amemaliza ziara yake huko Bethlehem, kando ya magharibi ya mto wa Jordan, na kuwasili Rome, Italia. Leo Rais Trump atakutana na rais Sergio Mattarella, na baadaye ataelekea Vatican kukutana na Papa Francis.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako