• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkakati wa China wa kujenga nchi yenye nguvu ya uzalishaji viwandani wavutia kampuni za kigeni

    (GMT+08:00) 2017-05-24 18:22:20

    China ilianza kutekeleza kwa pande zote mpango wa miaka kumi kuhusu mkakati wa kuwa nchi yenye nguvu ya uzalishaji viwandani mwaka 2015. Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China imefanya mkutano na waandishi wa habari ikisema, tangu ilipoanza kutekeleza mpango huo, China imepata maendeleo kwenye uzalishaji unaotumia akili bandia na uvumbuzi wa vifaa vya teknolojia ya hali ya juu. Wakati huo huo mkakati huo wa China umevutia kampuni nyingi za kigeni.

    Katika miaka miwili iliyopita, kazi mbalimbali za mpango huo wa miaka kumi kuhusu mkakati wa kujenga nchi yenye nguvu ya uzalishaji viwandani zimepata maendeleo makubwa, na kutoa mchango mkubwa katika kudumisha ongezeko la sekta ya viwanda na kuharakisha marekebisho ya uzalishaji. Naibu waziri wa viwanda na upashanaji wa habari wa China Bw. Xin Guobing amesema,

    "Kiwango cha uzalishaji unaotumia akili bandia kimeendelea kuinuka, mfumo wa vigezo umewekwa kimsingi, pia tumejenga viwanda vingi vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu. Utengenezaji kwa mujibu wa mahitaji na uzalishaji kwa ushirikiano wa utafiti vimepata maendeleo ya kasi."

    Vifaa vya safari za anga ya juu, miradi ya baharini, usafirishaji kwa njia ya reli ya kisasa ni sekta muhimu zilizotajwa kwenye mpango wa uongozi wa miaka kumi. Bw. Xin amesema, baada ya jitihada za miaka mingi, China imepata mafanikio makubwa kwenye sekta hizo.

    Wizara ya viwanda na upashanaji wa habari ya China hapo awali iliwahi kusema, mpango wa miaka kumi kuhusu mkakati wa kujenga nchi yenye nguvu ya uzalishaji viwandani pia unahusu kampuni za kigeni, na China inakaribisha kampuni za kigeni kushiriki kwenye ujenzi wa China. Imefahamika kuwa, tangu miaka miwili iliyopita, kampuni za kigeni zimeshiriki kwenye miradi mingi ikiwemo utengezaji wa vifaa vya teknolojia ya hali ya juu, uzalishaji usiosababisha uchafuzi, uzalishaji unaotumia akili bandia, na usafirishaji wa bidhaa wa kisasa. Bw. Xin pia ametaja mradi wa ndege kubwa ya aina ya C919 ambayo ilifanya safari kwa mara ya kwanza mwaka huu. Anasema,

    "Mradi huu ni mfano wa ushirikiano kati ya China na nchi nyingine. Mfano uko kwenye ijini, vifaa vya elektroniki, na mfumo wa udhibiti wa safari unaotengenezwa na kampuni nyingi za kigeni, zikiwemo kampuni za GE na Honeywell nchini Marekani. Baada ya kufanya safari ya kwanza kwa ndege hiyo, kampuni ya GE ilitoa habari ikitangaza kushiriki kwenye mradi huo."

     

    Bw. Xin pia amesema, baadhi ya nchi zilizoendelea bado zinaweka vizuizi katika kusafirisha teknolojia, vifaa na bidhaa nyingi kwa China, China inazitaka nchi hizo zifungue zaidi na kuimarisha ushirikiano na China, na China inakaribisha kampuni za nchi mbalimbali zishiriki kwenye mkakati wa kujenga China yenye nguvu ya uzalishaji viwandani.

      

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako