• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya sekta ya uongozaji safari kwa satilaiti nchini China yatazamiwa kuzidi yuan bilioni 400 katika miaka mitatu ijayo

    (GMT+08:00) 2017-05-24 18:51:49

    Mkutano wa 8 wa utaalamu wa mfumo wa uongozaji safari kwa satilaiti unamalizika kesho mjini Shanghai, na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 3000 kutoka hapa China na nchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa idara za usimamizi wa mfumo wa uongozaji safari kwa satilaiti, wataalamu, na wafanyakazi wa makampuni husika.

    Mkurugenzi wa ofisi ya mfumo wa uongozaji safari kwa satilaiti ya China Bw. Ran Cheng amesema kwenye mkutano huo kwamba, ifikapo mwaka 2020, thamani ya sekta ya uongozaji safari kwa satilaiti nchini China inatazamiwa kuzidi yuan bilioni 400.

    Kwenye mkutano huo China imetangaza chip inayosanifiwa na China kwa kujitegemea ambayo inaweza kuongoza safari kwa kasi na kutofautisha umbali ndani ya mita moja kwa kutumia satilaiti ya Beidou.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako