• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege Bombardier zaongeza watalii

    (GMT+08:00) 2017-05-24 19:54:32

    WIZARA ya Maliasili na Utalii imempongeza Rais John Magufuli kwa kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 na kuipa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

    Sekta ya utalii wa nje na ndani umeinuliwa na kuwapunguzia watalii wanaokuja gharama za usafiri kwa asilimia 50.

    Kulingana na waziri, wa sekta ya utalii, sekta hiyo, imeendelea kukua mwaka hadi mwaka na kwamba kwa mwaka wa fedha 2016/17, mapato ya sekta hiyo yaliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 1.9 hadi dola za Marekani milioni mbili.

    Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema kukua kwa utalii na kuongezeka kwa mapato yake kunatokana na kuongezeka kwa watalii wa nje ambapo mwaka 2015 walikuwa milioni 1.1 na 2016 milioni mbili.

    Mwezi ujao ndege zengine mbili za ziada zatarajiwa kununuliwa na zitakuwa na uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 270.

    Aidha amesema Bunge linaamini kufufuka kwa ATCL kutachangia kuongezeka kwa watalii watakaokuza biashara ya utalii na kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako