• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mali na Ghana zatinga fainali za AFCON U-17

    (GMT+08:00) 2017-05-25 09:34:08
    Timu ya taifa ya Mali ya vijana chini ya umri wa miaka 17 imeendeleza harakati zake za kutetea Ubingwa wake wa AFCON U-17 kwa kucheza dhidi ya Guinea katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya AFCON-U-17. Mali ambao ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo walilofanikiwa kutwaa mwaka 2015 katika ardhi ya Niger, wamefanikiwa kupata ushindi wa penati 2-0 dhidi ya Guinea, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa na mikwaju ya penati ikaamua mshindi.

    Ushindi wa Mali kwa kiasi kikubwa umechangiwa na golikipa wao Youssouf Koita ambaye amefanikiwa kucheza penati tatu za Guinea wakati moja ikitoka nje, ushindi huo sasa unaifanya Mali kucheza mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ghana May 28 wakati Guinea itacheza na Niger kutafuta mshindi wa tatu.

    Ghana nayo imetinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo.

    Na kikosi cha Serengeti Boys kimerejea Tanzania jana kikitokea Gabon na kupokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Dk Mwakyembe amewapongeza kutokana na walipofikia licha ya kwamba wameshindwa kutimiza ndoto ya kucheza Kombe la Dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako