• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kijiji cha Maerzhuang chatajirika kutokana na ufugaji wa kondoo

  (GMT+08:00) 2017-05-25 18:01:59

   

  Kwenye tafrija ya kuwakaribisha viongozi waliohudhuria mkutano wa kundi la nchi 20 (G20) uliofanyika mwaka jana huko Hangzhou, chakula kimoja cha nyama ya kondoo kilikaribishwa na viongozi wengi. Kondoo hao ni kutoka wilaya ya Yanchi mkoani Ningxia, China. Mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano kwenye wilaya hiyo, ameona kuwa kondoo wa huko wanafugwa kwenye mashamba yenye mazingira asili, na wakati fulani wanaweza kusikiliza muziki. Hivi sasa wakulima wengi wa huko wametajirika kutokana na ufugaji wa kondoo.

  Kijiji cha Maerzhuang cha wilaya ya Yanchi kiko kwenye sehemu inayounganisha jangwa na uwanda wa juu, ambacho kinakumbwa na ukame mara kwa mara. Kutokana na mazingira mabaya ya asili, ni vigumu kwa wanakijiji kudumisha maisha yao kwa kutegemea kilimo, hivyo kufuga kondoo kadhaa kulikuwa njia kuu ya kujipatia mapato.

  Kutokana na kuhimizwa na sera iliyotolewa na serikali ya China kuhusu kuwasadia watu maskini kuongeza mapato yao, kuanzia mwaka 2002, kijiji cha Maerzhuang kilianza kuufunga milima na kupiga marufuku ufugaji milimani. Baada ya miaka mitatu, mazingira ya asili ya huko yameboreshwa, na hali ya utoaji wa malisho yanayotumika kwa ufugaji pia imeboreshwa zaidi. Kijiji cha Maerzhuang kilianzisha shirikisho la ufugaji, na kuwahimiza wanakijiji wafuge kondoo kwa pamoja.

  Ili kuhakikisha wanakijiji wanapata mapatotulivu, na kuimarisha zaidi shughuli za ufugaji wa kondoo, serikali ya wilaya ya Yanchi kila mwaka imeweka mpango makini kuhusu maendeleo ya ufugaji wa kondoo, na imeongeza fedha maalumu, na kujenga kampuni na chama chenye nguvu ya ushindani sokoni.

  Kijiji cha Maerzhuang kimefanya ushirikiano na kampuni ya Xinhai kwa karibu mwaka mmoja, na nyama ya kondoo kwenye tafrija ya mkutano wa wakuu wa G20 ilitolewa na kampuni hiyo. Kijiji cha Maerzhuang kilitoa kondoo elfu 20 kwa kampuni ya Xinhai, na idadi hiyo ya mwaka huu itaongezeka zaidi.

  Ili kutafuta sifa nzuri zaidi ya kondoo, kampuni ya Xinhai ilijenga shamba la Ningxin, ambalo linafuga kondoo kwa njia ya kisayansi. Mkurugenzi wa shamba la Ningxin Bw. Feng Huan amesema, kondoo wa shamba hilo kuna wakati wanaweza kusikiliza muziki. Anasema,

  "Baada ya muda wa saa moja, tunaweka muziki kwa kondoo, kila alasiri tunafanya hivyo. Tumechagua nyimbo 15 kutoka nyimbo zaidi ya 300. Kondoo wakipenda wimbo fulani watakaribia spika inayocheza wimbo huo.."

  Kuhusu mustakabali wa ufugaji wa kondoo, Bw. Feng Huan amesema,

  "Naona watu wote wanaweza kujishughulisha na ufugaji wa kondoo, kampuni yetu ina matumaini kuwa tunaweza kuwaongoza wakulima wote wa huko kushughulikia ufugaji wa kondoo na kutajiri."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako