• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wenye nyumba Mwanza watakiwa kulipa kodi

    (GMT+08:00) 2017-05-25 18:52:01

    Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania(TRA) imewataka wakazi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kulipa kodi zao za majengo kabla ya Juni 30, mwaka huu.

    Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere wakati alipotoa maelezo ya majukumu ambayo mamlaka yake imepewa ya kukusanya kodi ya majengo kuanzia Julai mwaka jana, kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Mwanza.

    Alisema wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana) na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao ili kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili na kulipia kupitia benki yoyote ya biashara.

    Alisema TRA Mkoa wa Mwanza inasimamia kodi hiyo kwenye majengo yaliyokamilika au yanayotumika kwa makazi au biashara, yaliyopo kwenye maeneo yaliyopimwa au ambayo hayakupimwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako