Michuano ya kombe la dunia ya vijana chini ya umri wa miaka 20 inaendelea kushika kasi huko nchini Korea ya kusini ikiwa katika ngazi ya makundi.
Katika michezo ya kundi C wawakilishi wa Afrika timu ya Zambia walipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Iran. Nao Costa Rica wakatoshana nguvu na Ureno kwa Sare ya bao 1-1.
Kwenye kundi D Afrika ya kusini walichapwa na Italia kwa mabao 2-0, huku Uruguay wakiwafunga Japani kwa 2-0.
Michuano hiyo iliendelea tena jana katika kundi E ambapo Ufaransa ikajipatia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano baada ya kuibanjua Vietnam kwa magoli 4-0 na kuwafanya wawe vinara wa kundi lao, nao New Zealand baada ya kupepetana na Honduras wakaondoka na ushindi wa 3-1.
Katika kundi F Saudi Arabia wakapata ushindi wao wa kwanza baada ya kuwagaragaza Ecuador kwa 2-1. Nayo Marekani ikaongoza kundi baada ya kupambana na Senegal na kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |