• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka ya China yakabiliwa na kodi ya asilimia 100 kwa wachezaji wa nje

    (GMT+08:00) 2017-05-26 09:16:38

    Mamlaka ya Soka ya China inataka kutoza kodi ya asilimia 100 kwa klabu zinazowasaini wachezaji kutoka nje ya China ili kuhamasisha ushindani wa ndani. Lakini hatua hii kweli itatekelezeka? Rowan Simons ni mwandishi wa habari za soka za China na pia ni mwenyekiti wa klabu ya soka ya China, mtandao mkubwa wa soka wa ya ngazi ya chini ya China

    "Kama ikitekelezwa katika muundo wake wa sasa, na tukizingatia ukweli kwamba klabu zote za China zinapoteza pesa, kwa hiyo uingizaji wa wachezaji kutoka nje hapo baadaye, utakumbwa na kikwazo cha wachezaji kulipiwa kodi ya asilimia 100. Hivyo kwa hali kama hiyo itagharimu mara mbili ya uhamisho wa wachezaji kutoka nje, ambao idadi yao ni kubwa sana. Aidha sera hiyo itabadili nguvu ya wawekezaji kuvutia wachezaji hao. Wadhamini ambao wamekuwa wakivutiwa na ligi kwasababu ya wachezaji nyota, hata hivyo mamlaka inasema uingizwaji wa wachezaji hao umekuwa mkubwa mno, hivyo lazima kuwepo na njia za kudhibiti utoaji wa pesa nyingi kwa wachezaji wan je ili kutoa nafasi kwa wachezaji wa ndani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako