• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifaa vya usalama vilivyotolewa na China vyakabidhiwa kwa jeshi la Somalia

    (GMT+08:00) 2017-05-26 14:08:44

    Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimekabidhi vifaa vya usalama vilivyotolewa na China kwa jeshi la taifa la Somalia ili kusaidia operesheni za usalama nchini humo.

    Mwakilishi maalumu wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya Somalia Bw. Francisco Madeira amekabidhi majiko matatu yanayohamishika yenye uwezo wa kuwapikia askari mia sita. Vifaa vingine ni pamoja na vyandarua, helmeti za kuzuia risasi, na mahema, ambavyo vitatumiwa na jeshi la Somalia katika kambi zao.

    Mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Somalia Mohamed Ahmed Jimaale amesema, vifaa hivyo vitasaidia sana katika kuboresha mazingira ya maisha ya askari wa jeshi hilo katika kambi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako