• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatahadharisha huhusu mashambulizi ya kigaidi sehemu ya pwani

    (GMT+08:00) 2017-05-26 14:09:08

    Serikali ya Kenya imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kundi la Al-Shabaab kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Mombasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

    Kamishna wa kaunti ya Mombasa Bw. Evans Achoki amesema, polisi wamesambazwa katika kaunti hiyo ili kusaidia kuzuia vitendo vya kigaidi. Amesema wameimarisha usimamizi katika vituo muhimu ukiwemo uwanja wa ndege na maduka makuu, katika mlangobahari wa Likoni na mahoteli wakati wa kipindi cha Ramadhani na kwenye mikutano ya kisiasa.

    Pia amesema, idara za usalama zimefanikiwa kulidhibiti kundi la Al-Shabaab kwenye mji huo, lakini wakazi wa huko bado wanatakiwa kuchukua tahadhari na kubadilishana taarifa na mamlaka husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako