• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza umuhimu wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia ya Fuqing

    (GMT+08:00) 2017-05-26 17:04:28

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang amesema, mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Hualong Nambari 1 ni kazi muhimu katika kusukuma mbele mpango wa kitaifa unaoitwa "Imetengenezwa China Mwaka 2025". Mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia ya Fuqing ikiwa ni sehemu muhimu ya mradi wa Hualong Nambari 1, kumalizika kwa ujenzi wa kuba kwenye mitambo hiyo kuna umuhimu mkubwa.

    Bw. Li amesisitiza kwamba, ujenzi, uendeshaji na usimamizi wa vifaa vya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia unapaswa kuzingatia kwa makini usalama. Amesema anatarajia wafanyakazi wote wataendelea kujitahidi kukamilisha ujenzi huo kwa kuzingatia ubora na usalama.

    Pia amesema China inapenda kushiriki kwenye soko la kimataifa, kujitahidi kuwa nchi yenye nguvu ya uzalishaji umeme kwa nishati ya nyuklia duniani, na kutimiza uzalishaji viwandani wa hali ya juu nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako