• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maadhimisho ya 54 ya siku ya Afrika yafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-05-26 18:20:17

    Maadhimisho ya 54 ya siku ya Afrika yamefanyika katika kituo cha diplomasia ya umma hapa Beijing. Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika, naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Ming, waziri wa habari wa Guinea Bw. Mohamed Rachid N'Diaye, na watu kutoka sekta mbalimbali zaidi ya 500 walishiriki kwenye maadhimisho hayo.

    Balozi wa Madagascar nchini China Victor Sikonina amesema maadhimisho hayo si kama tu yanawasaidia watu kukumbuka historia ya Afrika, bali pia yanaionesha jumuiya ya kimataifa furaha ya nchi za Afrika kujipatia heshima na uhuru.

    Bw. Zhang Ming amesema ajenda ya Umoja wa Afrika kuelekea mwaka 2063 imeamua malengo na njia ya kutimiza maendeleo ya muda mrefu barani Afrika. China itashirikisha mipango 10 mikubwa ya ushirikiano kati ya China na Afrika na ajenda ya maendeleo ya Afrika, ili kuisaidia Afrika kutimiza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako