• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka jumuiya ya kimataifa iimarishe kuzuia migogoro ili kuwalinda raia wa kawaida

    (GMT+08:00) 2017-05-26 18:27:45

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi ameitaka jumuiya ya kimataifa iimarishe kinga na utatuzi wa mgogoro, ili kuhakikisha usalama wa raia wa kawaida, madaktari na vifaa.

    Bw. Liu Jieyi amesema hayo kwenye mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la kuwalinda raia, madaktari na vifaa kwenye mgogoro wa kijeshi.

    Bw. Liu amesema, kuwalinda raia wa kawaida ni jukumu la lazima kwa serikali za nchi husika na pande mbalimbali za mgogoro. Amesema, operesheni husika za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zimepewa jukumu la kuwalinda raia, na hii ni njia muhimu ya kuimarisha ulinzi wa raia. Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa linapaswa kufuata kwa makini majukumu yake linayopewa na umoja huo, na haliwezi kutekeleza majukumu ya kuwalinda raia, badala ya serikali za nchi husika na pande mbalimbali za mgogoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako