• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahusika wa sakata la mchanga wa madini kuchunguzwa na kushtakiwa

    (GMT+08:00) 2017-05-26 20:18:46

    Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) Bw Valentino Mlowola amesema watu wanaodaiwa kuhusika katika sakata la kuzembea kudhibiti biashara ya kusafirisha mchanga wa dhahabu nje ya nchi watachunguzwa na taasisi yake.

    Akizungumza mjini Dar es salaam, Mlowola amesema hata watendaji ambao walihusika kwenye sakata hilo na sasa hivi hawapo madarakani au wanashikilia nyadhifa nyingine, nao lazima watahojiwa na taasisi hiyo ili kufahamu sababu ya kuruhusu taifa kupata hasara kubwa kiasi hicho. Watendaji hao ni wanaofanya kazi wakala wa ukaguzi wa madini (TMAA), wizara ya nishati na madini na taasisi nyingine zinazohusika na madini. Ameongeza kuwa taasisi yake itashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuchunguza suala hilo na watakaobainika kuhusika wote watashtakiwa. Mlowola amesema wameshaanza kazi hiyo ambayo walipewa na rais kuwachunguza baadhi ya watumishi wa TMAA. Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi ambao hawakutaka kutajwa majina, walishangazwa na ripoti ya kamati maalum ya Rais juu ya ofisi za TMAA. Taarifa hii inakuja muda mchache tu baada ya rais Magufuli kumfuta kazi waziri wa nishati na madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kushindwa kuisimamia TMAA na kutoonesha juhudi za kujenga kinu cha kuchenjulia mchanga wenye mchanganyiko wa madini licha ya kuagizwa na sera ya madini ya mwaka 2009 tangu mwaka 2010.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako