• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kushamiri katika mfungo mwezi wa Ramadhani nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-26 20:19:19

    Biashara zinatarajiwa kushamiri kote nchini Kenya kufuatia kuanza kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhan kwa waislamu.Baadhi ya wafanya biashara waliozungumza na radio China Kimataifa wamesema tayari wameweka mikakati ifaayo ili kuhakikisha waislamu hawakosi chochote.Biashara inayoshamiri wakati huo ni ile ya uuzaji wa vyakula. Wakulima hivi sasa wameanza kuuza mazao yao kwa wingi ikiwa ni mojawapo ya hatua za kuwatosheleza kichakula ndugu zao wa kiislamu. Katika mji wa Mombasa baadhi ya wafanya biashara wanaojihusisha na vyakula walionekana wakiandaa vibanda vyao vya chakula kando kando mwa barabara ili kuwahudumia waislamu majira ya jioni. Baadhi ya wafanya biashara kutoka miji ya Meru na eneo la kaskazini mashariki wamesema watautumia vyema mwezi huu ili kuhakikisha juhudi zao zinazaa matunda kwa kupata faida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako