• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamiliki wa ardhi isiyotumika Tanzania kuanza kutoa kodi

    (GMT+08:00) 2017-05-26 20:20:02

    Serikali imetangaza kuanza kuwabana baada ya miezi sita, wamiliki wa viwanja vikubwa vilivyopo maeneo ya miji na majiji ikiwa hawaviendelezi kwa kuanza kuwatoza kodi ya ardhi hata kama vitakuwa havijapimwa.

    Tayari serikali hiyo imetangaza kuandaa miswada ya sheria ya uendelezaji miliki, Sheria ya Utwaaji Ardhi na Fidia na Sheria ya Mawakala wa Ardhi kudhibiti sekta ya udalali katika upangishaji wa majengo na uuzaji viwanja. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri William Lukuvi alisema watakaoshindwa kulipa kodi ndani ya mezi sita, viwanja vitataifishwa.

    Alisema bungeni Dodoma serikali imejipanga kuhakikisha kila ardhi iliyopo nchini inapimwa na kutumika kwa usawa na haki kama livyokusudiwa.Lukuvi amesema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakilia jinsi wanavyokandamizwa na madalali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako