• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya kugharamika zaidi kwenye uagizaji wa magari kutoka Japan

    (GMT+08:00) 2017-05-26 20:27:34

    Wakenya wanatarajiwa kugharamika zaidi katika ununuzi wa magari yaliyotumika kutoka Japana kama mpango wa kupunguza miaka ya magari yanayoagizwa kutoka nje itaidhinishwa.Jumuiya ya Afrika mashariki ilikuwa imependekeza miaka ya magari hayo kupunguzwa kutoka miaka minane hadi tano ifikapo mwaka wa 2021 ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kupiga jeki viwanda vya humu nchini.Kenya imeweka miaka ya magari yanayoagizwa kutoka njue kuwa miaka minane huku Tanzania ikiwa ni miaka 10. Rwanda, Burundi na Sudan Kusini hawajaweka wala kupisha sheria hiyo hivyo mtu anaweza kuagiza gari bila kujali ni la muda gani.Magari hayo ambayo yametumika ni maarufu sana nchini Kenya kutokana na gharama yake ya chini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako