• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la kimataifa la kupunguza umaskini la China wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-05-27 19:13:52

    Mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la kimataifa la kupunguza umaskini la China ulifanyika jana hapa Beijing, ambapo wajumbe 100 kutoka mashirika 16 ya kimataifa na nchi 7 walioshiriki walijadiliana kuhusu mifano mifumo ya kupunguza umaskini, na kujifunza uzoefu wa China katika sekta hiyo ili kuzisaidia nchi nyingine zinazoendelea kupata njia ya kuondokana na umaskini.

    Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya upunguzaji wa umaskini ya China Bw. Chen Zhigang amesema, kati ya mwaka 2013 hadi 2016, watu zaidi ya milioni 55 vijijini nchini China wameondokana na umaskini, hali hii imechangia utimizaji wa lengo la kupunguza watu maskini kwa milioni 10 kila mwaka kwa miaka minne mfululizo, na kuweka rekodi mpya katika historia ya kupunguza umaskini nchini China.

    Mjumbe wa Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa katika nchi za China na Korea ya Kaskazini anaona kuwa, China imefanikiwa kuwasaidia watu milioni 700 kuondokana na umaskini ndani ya miaka 30, hayo ni mafanikio makubwa sana. Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ni kupunguza umaskini, haitatimiza lengo hilo bila ya mchango huo uliotolewa na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako