• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano kati ya China na Kenya waingia kwenye njia ya kasi

    (GMT+08:00) 2017-05-29 08:05:21

    Reli ya SGR kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ni reli ya kwanza iliyojengwa tangu Kenya ipate uhuru, inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu. Reli hiyo inayoitwa na wakenya "ujenzi wa milenia" imejengwa kwa kufuata vigezo vya kichina, na inabeba ndoto ya watu wa vizazi vilivyopita vya Kenya, na kusaidia kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya Afrika Mashariki kuingia kwenye njia ya kasi.

    Baada ya siku kadhaa, treni ya kwanza itafunga safari kutoka Nairobi kuelekea Mombasa, bandari kubwa zaidi Afrika Mashariki. Reli hiyo inaunganisha miji hiyo miwili mikubwa, ambayo pia ni mwanzo wa mradi mkuu wa ujenzi wa mtandao mpya wa reli Afrika Mashariki. Ofisa wa mradi wa ujenzi wa reli ya SGR katika shirika la reli la Kenya Bw. Davis Mwaberia, amesema reli hiyo yenye urefu wa kilomita 472, treni yake ya abiria itakuwa na kasi ya kilomita 120 kwa saa, huku mwendo wa usafirishaji wa mizigo ni kilomita 80 kwa saa, mizigo inaweza kufikia uzito wa tani milioni 25. Mradi mzima umejengwa kwa kutumia kigezo cha kiwango cha juu zaidi kinachotumiwa na ujenzi wa reli nchini China, ambayo inaambatana na mfumo wa aina ya kisasa wa usimamizi.

    Mwaka 2012 mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliamua kujengwa kwa reli ya kisasa inayotakiwa kuchukua nafasi ya reli ya zamani ambayo ilijengwa na waingereza mwishoni mwa karne ya 19. Mwanahistoria Bw. Musa Mwarua anayetoka Chuo Kikuu cha Kenyatta anajulisha kuwa, Waingereza walijenga reli ya zamani kutoka Mombasa hadi ziwa Victoria kwa kupitia Nairobi yenye gharama za Pauni milioni 5.5, lakini sio kwa lengo la kusaidia maendeleo ya sehemu zilizopita reli hiyo. Lengo kuu la wakoloni lilikuwa ni kulidhibiti ziwa Victoria, ambalo ni ziwa kubwa la pili la maji baridi lenye eneo la kilomita karibu elfu 70 za mraba, chanzo cha Mto Nile, hivyo waingereza walitaka kudhibiti eneo zima la Afrika Mashariki kwa kujenga reli hii .

    Lakini miaka mia moja imepita, reli hiyo imezeeka kiteknolojia na kimitambo, hata haiwezi kukidhi mahitaji ya usafirishaji wa abiria wala mizigo kati ya Nairobi na Mombasa. Licha ya kuwa bado inafanya kazi, lakini inachukua muda wa saa 15 ya kumaliza umbali wa kilomita 530, kasi ni kilomita 40 kwa saa. Wakati huohuo, treni inachelewa mara kwa mara, na muda halisi unaotumiwa huwa ni mara moja zaidi.

    Ujenzi wa reli ya SGR unaonesha moyo wa ushirikiano wa China na Kenya. Bibi Carole Kariuki, mkurugenzi mkuu wa Muungano wa wafanyiabiashara wa kibinafsi (KEPSA) anaeleza, kampuni ya ujenzi ya China inafuatilia sana kulinda maslahi ya wafanyakazi wa Kenya, inatumia sera ya usawa isiyo ya kibaguzi, na kusimamia vizuri kuwaajiri wafanyakazi wenyeji.

    Wachina wanasema kuwasaidia wengine kwa kuwafundisha kuvua samaki, ni vizuri zaidi kuliko kuwapa samaki. Mbali na kutoa mafunzo wakati wa kujenga reli ya SGR, kampuni ya ujenzi ya China vilevile inazingatia sana kuwafundisha watu wanaoendesha na kusimamia reli hiyo. Kampuni ya Barabara na daraja ya China imeshirikiana na Chuo Kikuu cha Kusini Magharibi cha China na vyuo vingine, kutoka mafunzo kwa wanafunzi wa Kenya. Chuo cha reli ya Kenya cha urafiki kati ya China na Afrika pia kinapangiwa kujengwa, lengo lake ni kuisaidia Kenya kuanzisha masomo ya mradi wa ujenzi wa reli nchini Kenya, na kuchangia kuimarisha uwezo wa nguvukazi ya wakenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako