• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fainali za Kombe la Shirikisho Tanzania: Simba mabingwa kombe la Shirikisho

    (GMT+08:00) 2017-05-29 10:50:03
    Klabu ya soka ya wekundu wa msimbazi Simba Sports Club imetwaa ubingwa wa kombe la shirikisho la TFF baada ya kuinyuka Mbao FC bao 2-1 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa kunako dimba la Jamhuri mkoani Dodoma.

    Fainali hiyo iliyokuwa na ushindani wa hali ya juu, timu zote mbili zimepata mabao katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika pasipo kufungana.

    Mabao ya Simba yamefungwa na Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya, bao la kufutia machozi la Mbao FC limefungwa na Robert Ndaki. Kwa ushindi huo Simba imakata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2012/13.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako