• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la FA Uingereza: Arsenal yatwaa ndoo kwa kuifunga Chelsea

    (GMT+08:00) 2017-05-29 10:54:32

    Arsenal imetwaa FA CUP baada ya kuwachapa Mabingwa wa England Chelsea 2-1 katika Fainali iliyochezwa Uwanja wa Wembley Jijini London.

    Kombe hilo huenda litaleta ahueni klabuni hasa baada ya kumaliza nafasi ya 5 kwenye ligi kuu ya Uingereza (EPL) na kukosa kucheza UEFA Champions Ligi kwa mara ya kwanza katika miaka 20 na msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI.

    Arsenal walifunga bao dakika ya 4 tu kupitia Alexis Sanchez goli ambalo halikukubaliwa moja kwa moja baada refa msaidizi kuinua kibendera kuashiria Aaron Ramsey alikuwa Offside na refa Anthony Taylor kulazimika kwenda kuongea nae na baada ya hapo kuashiria ni goli halali.

    Hadi half time Arsenal ilikuwa ainaongoza kwa goli 1-0, kipindi cha pili, Chelsea ilifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 76 kupitia Diego Costa lakini lilidumu kwa dakika 3 kabla ya Aaron Ramsey kufunga goli la pili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako