• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sikukuu ya Duanwu yaweka shinikizo kwa usafiri wa treni nchini China

    (GMT+08:00) 2017-05-29 18:29:27

    Sikukuu ya Duanwu iliyoanza kusherehekewa jana mpaka kesho imeweka shinikizo kubwa kwenye mfumo wa safari za treni za abiria nchini China, kwa kuwa watu wengi zaidi wanapendelea kutumia usafiri huo.

    Shirika la reli la China limesema, safari milioni 12.1 za treni zimefanyika hapo jana, ikiwa ni zaidi kwa asilimia 8.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Shirika hilo limesema litaongeza treni 253 hii leo, ambapo safari za treni za abiria milioni 9.1 zinatarajiwa kufanyika.

    Sikukuu ya Duanwu ni sikukuu ya jadi nchini China, na inasherehekewa kila tarehe tano ya mwezi wa tano katika kalenda ya kilimo ya kichina, ambayo mwaka huu inaangukia siku ya kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako