• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili wa karne 21 wa Panglong wa Myanmar wafikia makubaliano ya muungano wa majimbo

    (GMT+08:00) 2017-05-29 18:57:29

    Mkutano wa pili wa karne 21 wa Panglong wa Myanmar umefungwa leo, na wajumbe wa pande mbalimbali wamesaini nyaraka za makubaliano ya muungano wa majimbo zenye vifungu 37.

    Akizungumza kwenye mkutano huo, Mshauri wa Taifa la Myanmar, Aung San Suu Kyi amepongeza kuingizwa kwa kanuni 37 kwenye makubaliano ya pamoja. Amesema hiyo ni hatua muhimu kuelekea amani, mwafaka wa kitaifa na kuanza kwa umoja wa kidemokrasia nchini humo.

    Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe kutoka makundi manne makuu ambayo ni pamoja na bunge, jeshi, vyama vya kisiasa na makundi yenye silaha wamesaini vifungu 37, ambavyo vitakuwa sehemu ya toleo la mwisho la makubaliano ya amani ya muungano wa majimbo yatakayoleta amani ya kudumu katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako