• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Stars kuweka kambi Misri, kujiandaa AFCON 2019

    (GMT+08:00) 2017-05-30 08:45:02
    Kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kinatarajiwa kuondoka leo jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenda Misri.

    Taifa Stars ambayo inaenda kuweka kambi ya siku 8 kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Wachezaji 21 kutoka Tanzania wataungana na wachezaji wengine 2, Nahodha Mbwana Samatta na Faridi Mussa wanaocheza soka la kulipwa ulaya.

    Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika kundi L kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako