• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya ujenzi ya China inayoshughulikia ujenzi wa SGR nchini Kenya yatangaza ripoti ya majukumu ya jamii

    (GMT+08:00) 2017-05-30 18:25:16

    Wakati Reli ya SGR ya kutoka Mombasa-Nairobi nchini Kenya inakaribia kuanza kazi rasmi, kampuni ya ujenzi ya China iliyoshughulikia ujenzi wa reli hiyo iliandaa mkutano na kutoa ripoti ya majukumu ya jamii ya mwaka 2016 na ya mradi wa reli ya SGR mjini Nairobi, Kenya. Hii vilevile ni mara ya kwanza kwa kampuni ya China kuandaa mkutano kama huu nje ya China.

    Reli ya SGR ni mradi muhimu katika mpango wa mwaka 2030 wa Kenya, pia ni kituo muhimu cha mtandao wa reli kwa Afrika Mashariki katika siku za baadae. Ripoti ya majukumu ya jamii ya mwaka 2016 ya reli ya SGR yenye zaidi ya kurasa 90 inaeleza jinsi mradi huo ulivyozingatia athari mbalimbali kwa pande zinazohusika katika hatua za ubunifu, ujenzi na uendeshaji, kuheshimu haki za kibinadamu, na kufuata kanuni na sheria, ili kuhakikisha mradi huo unachangia katika maendeleo ya uchumi, uhifadhi wa mazingira, na masikilizano ya jamii. Takwimu zinaonesha kuwa, madaraja 88 yenye urefu wa kilomita 30 kati ya kilomita 472 za reli hiyo, na kalvati 969 zimejengwa katika reli zenye umbali wa kilomita 170 zinazopita kwenye eneo la hifadhi za wanyama. Wakati wa ujenzi huo, mradi huo umetoa nafasi elfu 46 za ajira kwa Wakenya na kuwaandaa wataalamu wenyeji elfu 18.

    Balozi wa China nchini Kenya Bw. Liu Xianfa ameeleza kuwa, ni njia ya lazima kwa kampuni za China kubeba majukumu ya jamii ili kutimiza maendeleo ya pamoja tena kwa kasi zaidi.

    Naibu waziri wa mawasiliano, miundombinu, nyumba na maendeleo ya miji ya Kenya Paul Maringa Mwangi amesema, ujenzi huo umechangia ongezeko la mauzo ya saruji, mbao na zana mbalimbali, aidha wenyeji wengi wa huko wamepewa mafunzo ya kiufundi, hayo yote yameonesha dhahiri kampuni hiyo ya China imetoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. Naibu waziri wa elimu ya Kenya Richard Belio Kipsang amesema, ujenzi huo umesaidia katika kuinua kiwango cha uwezo wa kazi na kiufundi wa huko na kutoa fursa nyingi kwa wanafunzi wa huko kupata uzoefu halisi na kuongeza uwezo wa ushindani. Mkurugenzi wa Idara ya uhifadhi wa mazingira wa Kenya Geofrey Wahungu ameeleza kuwa reli hiyo imetoa mfano mzuri kwa Kenya hata nchi za Afrika Mashariki katika mambo ya ubunifu, utekelezaji wa miradi ya aina hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako