• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guangzhou kubadili mabasi yote ya abiria mjini humo na magari yanayotumia nishati safi ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2017-05-30 18:33:47

    Mji wa Guangzhou umeanza kubadili maelfu ya mabasi yake ya abiria yanayotumia petroli kwa mabasi yanayotumia nishati safi ya kijani.

    Kutokana na mpango huo mpya, itakapofika mwaka 2020, mabasi yote yanayotumia petroli na dizeli yatabadilishwa na mabasi yanayotumia umeme, ikimaanisha kuwa mji wa Guangzhou utakuwa na magari elfu 30 yanayotumia nishati safi ikiwemo mabasi na teksi.

    Mpango huo mpya unaonyesha kuwa, idadi ya maegesho ya magari yenye maeneo ya kuchajia magari itachukua asilimia 30 ya maeneo ya kuegesha magari katika majengo ya ofisi, maduka makubwa, na migahawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako