• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia:Ethiopia yaelekea kuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2017-05-30 18:46:09

    Ethiopia sasa imeiondoa rasmi Kenya kama kituo kikuu cha biashara Afrika Mashariki.

    Takwimu kutoka kwa shirika kuu la fedha duniani zinaonyesha kwamba pato la taifa la Ethiopia, limefikia dola bilioni 78 kutoka bilioni 72.

    Uchumi wa Ethiopia umekuwa kwa asilimia 10.8 kuanzia mwaka 2015 na nchi hii sasa imeingiza dola milioni 29 zaidi ikilinganishwa na Kenya.

    Mchango mkubwa wa uchumi wa Ethiopia unatokana na miundo msingi na uwekezaji.

    Uchumi wa Ethiopia umekuwa ukiimarika tangu mwaka 2015 kutokana na reli na miradi ya kuzalisha kawi.

    Hivi karibuni,Ethiopia imetangaza faida kubwa kutoka kwa uuzaji wa kawi katika nchi za Sudan na Djibouti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako