• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Wananchi kuwezeshwa kiuchumi

    (GMT+08:00) 2017-05-30 18:46:36

    Barazala la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limesaini mkataba wa ushirikiano na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa mapana zaidi.

    Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji NEEC, Beng'i Issa alisema kampuni hiyo itakuwa mshirika wao na mchapishaji rasmi wa shughuli zote wanazozifanya katika masuala ya uwezeshaji.

    Alisema baraza linaamini katika mtandao mpana, uzoefu na uimara wa taasisi hiyo kupitia mitandao yake ya habari, litawafikia Watanzania wengi zaidi ndani na nje ya nchi katika kuhamasisha kuhusu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

    Mwaka huu watafanya Kongamano la Pili la NEEC mjini Dodoma, ambalo litakutanisha wadau wa sekta ya umma na binafsi nchini, kujadiliana kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo.

    Kongamani hilo litachochea kasi ya utekelezaji wa mikakati ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na kujifunza kutoka kwa wadau mbalimbali namna bora zaidi ya kusukuma mbele gurudumu la uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini.

    Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi aliishukuru NEEC kwa kuona fursa ambayo ipo kwa kutumia Kampuni ya Magazeti ya Serikali na kuwahakikishia kuwa wamepata chombo muafaka ambacho kitapeleka taarifa za uwezeshaji kwa mapana kwa ajili ya kuwezesha wananchi kushiriki katika uchumi wa nchi na dunia kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako