• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tanzania kunufaika na ziara ya marais

    (GMT+08:00) 2017-05-30 18:46:58

    Wizaraya ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki imebainisha faida za ziara za viongozi wa kimataifa takribani 10 nchini pamoja na wajumbe mbalimbali kutoka nchi za nje, ambao wamefanikisha kusainiwa kwa mikataba takribani 40 ya miradi ya maendeleo.

    Pamoja na hayo, wizara hiyo imesema Umoja wa Mataifa umepongeza juhudi za Rais John Magufuli, kutekeleza vyema kanuni za utalawa bora ndani na nje ya nchi. Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

    Alisema ujio wa viongozi na wajumbe hao nchini, umeiwezesha Tanzania kuimarisha uhusiano wake na nchi za viongozi hao kiuchumi, kijamii na kiusalama. Aliwataja viongozi waliofanya ziara kuanzia mwaka jana na mwaka huu kuwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi aliyewasili nchini Julai mwaka jana, na kufanikisha nchi yake kuipatia Tanzania mkopo wa riba nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500.

    Balozi Mahiga pia alifafanua ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayeshughulikia masuala ya Afrika na kubainisha kuwa kupitia ziara hiyo, Serikali ya Iran ilikabidhi msaada wa vifaa kwa Chuo cha Ufundi Stadi Mkokoton Zanzibar wenye thamani ya Dola za Marekani 500,000.

    Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliyefanya ziara yake nchini Februari Mwaka huu, naye kupitia ziara hiyo Tanzania na Uganda zilisaini hati za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kisiasa, sekta ya biashara na uwekezaji, uchukuzi, mafuta na nishati.

    Ziara nyingine ni ziara ya Waziri Mkuu wa Shirikisho la Kidemorasia la Jamhuri ya Ethiopia, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes. Wengine ni Waziri wa Biashara za Kimataifa na Maendeleo wa Jamhuri ya Finland na ziara ya Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Uswisi na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.

    Balozi Mahiga, kupitia ziara hizo katika kipindi cha mwaka 2016/17 wizara hiyo iliratibu na kusimamia kusainiwa kwa mikataba 12 na hati ya za makubaliano 28 baina ya Tanzania na nchi nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako