• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Kenya wapongeza uzinduzi wa Reli ya SGR

    (GMT+08:00) 2017-05-30 19:22:14

    Kesho reli ya SGR inayounganisha Mombasa na Nairobi itazinduliwa rasmi, maofisa wa Kenya wamepongeza uzinduzi wa reli hiyo huku wakisema reli hiyo italeta nguvu mpya kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Kenya.

    Waziri wa uchukuzi na miundombinu wa Kenya Bw. James Macharia amesema, baada ya reli hiyo kuzinduliwa, muda wa usafirishaji wa mizigo unatarajiwa kupungua kutoka siku mbili kwa kutumia barabara hadi saa 8 kwa treni, ambao unamaanisha kupunguza gharama kwa kampuni za uchukuzi. Licha ya usafirishaji wa mizigo, reli hiyo pia itaanzisha treni ya abiria, ambayo italeta chaguo jipya kwa wakazi wa huko.

    Katibu wa kudumu wa wizara ya uchukuzi na miundombinu Bw. Paul Maringa Mwangi amesema, , ujenzi wa reli hiyo umeleta ongezeko la biashara kwa kampuni zaidi ya 934 za kutengeneza saruji na mbao na ugavi wa vifaa , na wakandarasi zaidi ya 300 walishiriki kwenye mradi huo. Hii inamaanisha kuwa mradi huo umetoa mchango mkubwa katika kuhimiza uchumi wa huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako