• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barelona yamtangaza Ernesto Valverde kocha mpya

    (GMT+08:00) 2017-05-31 08:41:03

    Timu ya Barcelona imemteua Ernesto Valverde kuwa Kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka miwili wenye nyongeza ya mwaka mmoja. Valverde, mwenye Miaka 53, alikuwa forward wa zamani wa Barca aliyechezea klabu hiyo kwa misimu miwili kuanzia 1988 na kufunga magoli 8 katika mechi 22 akiandamwa na majeruhi. Kocha huyo ametokea Athletic Bilbao alikokuwa kocha mkuu na kujiuzulu wiki iliyopita na sasa anachukua nafasi ya Luis Enrique ambae amemaliza mkataba wake wa miaka mitatu na kuiweka Barca nafasi ya pili kwenye La Liga wakiwa nyuma ya mabingwa Real Madrid. Akitangaza ujio wa Ernesto Valverde ambae atatambulishwa rasmi Alhamisi, Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, alimsifia Valverded na kudai anakuza vijana na anacheza staili ya Barcelona.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako