• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la reli la Kenya lasaini makubaliano na kampuni ya China kuhusu uendeshaji wa reli

  (GMT+08:00) 2017-05-31 09:33:14

  Shirika la reli la Kenya KRC na kampuni ya CRBC ya China wamesaini makubaliano ya usimamizi, ukarabati na huduma kuhusu reli iliyozunduliwa ya Mombasa-Nairobi.

  Mkurugenzi wa KRC Bw Atanas Maina amesema sehemu muhimu za reli hiyo zitaendeshwa na kampuni ya CRBC kwa mujibu wa matakwa ya shirika la reli la Kenya, kampuni hiyo pia itahusika na kazi ya matunzo ya vifaa na reli, ili kuhakikisha kuwa vifaa vinatunzwa na kuwa katika vigezo vizuri vya kimataifa.

  Bw Maina amesema wameichagua kampuni hiyo kusimamia reli hiyo kwa sababu ni kampuni iliyojengwa reli hiyo na ina uwezo wa kufanya kazi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako