• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Treni ya SGR ya kutoka Mombasa-Nairobi iliyojengwa kwa msaada wa China yazinduliwa rasmi

    (GMT+08:00) 2017-05-31 19:28:30

    Siku moja tu baada ya kuzindua treni ya mizigo rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua tena treni ya kisasa ya abiria iliyojengwa kwa msaada wa China.

    Ilikuwa ni siku ya ambayo kila mkenya alikuwa anaisubiri kwa hamu ambapo wengi wao walifika kujionea wenyewe matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na wachina ya kurahisisha shughuli za usafiri nchini Kenya. Akizungumza baada ya kuizindua rasmi treni ya abiria rais Uhuru Kenyatta ameitaja treni hiyo kuwa ya mwananchi wa kawaida inayolenga kumpunzia gharama za usafirishaji. Ameongeza kuwa nauli kwa mwananchi wa kawaida haitakuwa zaidi ya shilingi 700 za Kenya.

    Uzinduzi huo unakuja siku moja tu baada ya shirika la reli la Kenya KRC na kampuni ya CRBC ya China ambayo ndiyo iliyojenga reli hiyo ya kisasa kusaini makubaliano ya usimamizi, ukarabati na huduma kuhusu reli hiyo inayotoka Mombasa hadi Nairobi. Kampuni hiyo pia itahusika na kazi ya matunzo ya vifaa na reli, ili kuhakikisha kuwa vifaa vinatunzwa na kuwa katika vigezo vizuri vya kimataifa. Kenya imeamua kutobaki nyuma kati ya nchi marafiki wa China, kunufaika na miradi ya kiwango cha juu kama vile ujenzi wa reli za kisasa, barabara na nyinginezo. Aidha rais Kenyatta ameahidi kupiga jeki uhusiano na ushirikiano kati ya Kenya na China.

    Kuna mifano mingi iliyo hai ya reli zilizojengwa na makampuni ya China kama mradi wa reli ya Kaduna- Abuja wa nchini Nigeria wenye kilomita 187, na mradi wa ujenzi wa reli ya usafiri wa umma mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia AA-LRT, miradi ambayo tayari imeanza kufanya kazi na kuwanufaisha wa tu wa nchi hizo.Bwana Wang Yong ni mjumbe wa taifa la China. Anautaja mradi wa SGR kuwa ishara ya kwanza ya mavuno ya mpango wa ukanda mmoja na njia moja ulioanzishwa na rais Xi Jinping. Alisema:"Mradi wa SGR ishara ya kwanza ya mavuno ya mpango wa ukanda mmoja na njia moja ulioanzishwa na rais Xi Jinping na pia ni sehemu ya mipango 10 ya ushirikiano iliotangazwa wakati wa mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC mjini Johannesburg. Pia ni mradi mkuu na muhimu katika ushirikiano wa China na Afrika wa kuendeleza mshikamano wa kikanda kwa njia ya reli, usafiri wa anga na barabara ambazo zitakuza uwezo wa kiviwanda wa Afrika. Huu ndio mradi mkubwa zaidi nchini Kenya na pia sehemu ya ruwaza ya Kenya ya kiuchumi ya mwaka 2030. Reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi ni kiungo muhimu katika sekta ya uchukuzi wa reli katika katika kanda ya Afrika mashariki na ni ishara ya urafiki wa enzi mpya kati ya Kenya na China inayoonyesha manufaa ya pande mbili. Reli hii itasaidia kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye kanda ya Afrika mashariki."

    Kwenye uzinduzi huo pia tulipata fursa ya kuzungumza na wakenya mbali mbali na walionekana kuwa na matarajio makubwa kuhusu treni hizo mpya zilizozinduliwa.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako