WIZARA ya Fedha na Mipango imesema mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 ni kuendelea kukua na kutengemaa kwa uchumi kwa asilimia saba, kuimarika kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani na mfumuko wa bei.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, changamoto zilizoikabili serikali katika kipindi hicho cha 2016/17 zimetajwa kuwa ni mwamko mdogo wa kulipa kodi, kuchelewa kupatikana kwa mikopo ya masharti nafuu ya kibiashara kutoka nje na kuchelewa kupatikana fedha kutoka kwa washirika.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amebainisha haya, wakati akiwasilisha bungeni, Bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.
Dk Mpango amesema kuanzia mwaka jana hadi Machi mwaka huu, kasi ya uchumi imeendelea kuwa ya kuridhisha na kubakia katika wastani wa asilimia saba.
Ukuaji wa kasi umetokana na shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |