• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Wasagaji Nafaka Waonya Bei Ya Unga Huenda Ikaongezeka

    (GMT+08:00) 2017-05-31 20:01:15

    Huenda bei ya unga wa mahindi ikaongezeka kutokana na kutokuwepo kwa usambazaji dhabiti wa bidhaa hiyo na serikali wasagaji nafaka wameonya.

    Mwenyekiti wa muungano wa wasagaji nafaka Nick Hutchinson ameliambia bunge kwamba kwa sasa hawana bidhaa hiyo na wanategemea mahindi yaliyonunuliwa kutoka nje ya nchi.

    Unga uliopunguzwa bei na serikali ulipaswa kuwepo hadi Septemba 30.

    Muungano huo umeiambia kamati ya bunge kuhusu kilimo kwamba walikua na magunia laki moja na kumi katika hifadhi yao wakati waliopotoa onyo mwezi Aprili kuhusu uhaba wa bidhaa hiyo.

    Kwa upande wa waziri wa maji Eugene Wamalwa ameiambia kamati hiyo kwamba uhaba wa chakula nchini umesababishwa na serikali kukosa kuwekeza katika unyunyizaji maji mashamba ili kuwepo na usambazaji thabiti wa bidhaa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako